Mali-Ufaransa

Raia wa Ufaransa mshukiwa wa ugaidi unaofanyika nchini Mali Gille le Guen akamatwa

Raia wa Ufaransa aliyeshukiwa kuwa mfuasi wa kundi la kigaidi baada ya kuonekana katika picha ya Video akiionya Ufaransa juu ya uvamizi wake nchini Mali, amekamatwa na Vikosi vya Ufaransa kaskazini mwa Mali.

Diarra / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Chanzo cha Habari cha Serikali ya Mali kimethibitisha kimethibitisha kukamatwa kwa raia huyo wa Ufaransa .

Gille le Guen ambaye anajulikana kwa jini la Abdel Jelil aliyekamatwa karibu na mji wa Timbuktu mwishoni mwa juma, atahojiwa nchini Mali kabla ya kusafirishwa kupelekwa nchini Ufaransa.

Mtu huyo anaaminika kuwa mfuasi wa Alqaeda wa AQIM baada ya yeye na Familia yake kuhamia nchini Mali akitokea nchini Morocco na Mauritania ambapo pia aliwahi kuishi.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanaeleza kufanikiwa kwa jitihada za vikosi vya Ufaransa kupambana na wanamgambo wa kiislamu kaskazini mwa Mali.

Umoja wa Mataifa upo mbioni kupeleka jeshi la kimataifa nchini Mali ili kuchukua nafasi ya wanajeshi ya Ufaransa ambao tayari wameshaanza kuondoka nchini humo.