SOMALI-UN

Njaa yatikisa na kuua watu 260,000 nchini Somalia, Umoja wa Mataifa ulichelewa kuchukua hatua

RFI

Wananchi wasiopungua 260,000 wamefariki kutokana na njaa nchini Somalia kati ya mwaka 2010 na 2012 nusu kati yao ni watoto walio chini ya umri wa miaka mitano na njaa inaendelea kuwa tishio nchini humo na pembe ya Afrika kwa ujumla. 

Matangazo ya kibiashara

 

Ripoti ya Serikali imethibitisha kutokea kwa vifo hivyo huku Umoja wa Mataifa, UN ukikiri kuwa ulipaswa kufanya jitihada zaidi za kujiandaa kukabiliana na njaa nchini Somalia ili kuepusha vifo kama hivyo.
 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo njaa na chakula kutokua salama ndiyo chanzo cha vifo hivyo na Umoja wa Mataifa ulichelewa kutoa tahadhari ya njaa hiyo ambayo imeteza uhai wa wananchi wengi.
 

Katika kipindi hicho cha njaa mwezi Julai mwaka 2011 kilikua kipindi kigumu zaidi cha ukame ambao uliathiri kwa kiasi kikubwa katika eneo la pembe ya Afrika ambapo watu wapatao milioni kumi na tatu.
 

Njaa nchini Somalia ilitangazwa rasmi mnamo mwezi Julai mwaka 2011 katika mikoa ya Bakool kusini na Shabelle chini lakini baadaye ilisambaa mpaka katika mikoa ya Shabelle Kati, Agoye na Mogadishu.