KOREA KASKAZINI-MAREKANI

Raia wa Marekani afungwa jela miaka 15 nchini Korea Kaskazini na kazi za sulubu

RFI

Mahakama Kuu nchini Korea Kaskazini imemhukumu kifungo cha miaka kumi na tano jela pamoja na kazi za sulubu raia wa Marekani Pae Jun-Ho anayetambulika kwa jina la Kenneth Bae huko Washington kwa kosa lakuchochea uadui.

Matangazo ya kibiashara

Bae ambaye alikuwa muongozaji wa watalii wa Korea na Marekani amekutwa na hatia na Mahakama Kuu na kupewa adhabu hiyo kitu ambacho kinaongeza uadui baina ya Pyongyang na Washington.

Hatua hiyo inadaiwa itaongeza uhasama zaidi baina ya nchi za Korea Kaskazini na Marekani ikizingatiwa kuwa nchi hizo bado ziko katika mvutano mkali kuhusu mtafaruku wa Korea Kusini na washirika wake.

Wakati huohuo Mamlaka nchini Marekani zimetoa picha zinazowaonesha watu watatu wanaotajwa kuwepo wakati shambulizi la bomu likitokea katika Ubalozi wake nchini Libya kwenye Mji wa Benghazi na kuwataja kama watuhumiwa kwenye tukio hilo.
 

Kitengo cha Uchunguzi nchini Marekani FBI kimesema kinataka kuwahoji watu hao kuona kama wanaweza wakasaidia kupatikana kwa wale waliohusika kwenye shambulizi lililosababisha kifo cha Balozi wake Chris Stevens.
 

Serikali ya Marekani imetoa wito kwa watu wenye ushahidi au maelezo ya ziada yanayoweza kusaidia kwenye uchunguzi huo kuwasilisha maelezo yao kwa FBI ili kuweza kuwanasa waliohusika.