UMOJA WA MATAIFA

Umoja wa Mataifa wataka Serikali, Mashirika kulinda usalama wa waandishi wa habari

Dunia hii leo inaadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari huku Changamoto kadhaa zimekuwa zikijitokeza Duniani dhidi ya Wanahabari vikiwemo vitendo vya mauaji dhidi ya Wanahabari.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon alitoa kauli yake katika Maadhimisho ya miaka 20 ya Uhuru wa vyombo vya habari chini ya Kauli mbiu “usalama wakati wa kuongea” “hakikisha usalama wa Wanahabari na Wafanyakazi wa vyombo vya habari”
 

Ban amesema kuwa Wanahabari wamekuwa wakipambana na vikwazo kutoka kwa Serikali, Mashirika, Makundi ya Uhalifu, wanamgambo na wengine ambao hufanya kazi za wanahabari kuwa ngumu.
 

Siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari ambayo huadhimishwa mwezi Mei 3 kila mwaka ilitangazwa rasmi na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mwezi Desemba mwaka 1993.
 

Siku hiyo ilianzishwa kufuatia mapendekezo ya UNESCO ili kuweza kutathimini taabu na Changamoto wazipatazo Wanahabari na Wafanyakazi ndani ya Vyombo vya Habari.
 

Waaandishi wa habari wamekua wakifanya kazi katika mazingira magumu na hatarishi hali ambayo husababisha vifo na kujeruhiwa wakiwa katika utekelezaji wa majukumu yao.
 

Ripoti mbalimbali za kimataifa zinaonyesha kuwa mwandishi mmoja hufa kila baada ya siku tano katika nchi mbalimbali duniani tangu mwaka 1992 mpaka sasa.