JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-DRC-TANZANIA-BURUNDI

Waandishi waadhimisha Uhuru wa Vyombo vya Habari wakikabiliwa na tishio la usalama wao

RFI

Wakati dunia inasherehekea siku ya uhuru wa Vyombo vya Habari wana habari nchini Afrika ya Kati wanaripotiwa kukumbwa na vitendo vya kunyanyaswa huku baadhi wakikamatwa na kutishiwa maisha wapiganaji waasi wa Seleka. 

Matangazo ya kibiashara

Ambroise Pierre ni mwenyekiti wa Shirika la Maripota wasio na mipaka anasema wanahabari Huko Bangui wanafanya kazi katika mazingira hata rishi.
 

Ameongeza kusema kuwa katika siku za hivi karibuni wanahabari hao waliomba serikali ya raisi wa nchi hiyo Michel Djotodia kuwapa Ulinzi wa kutosha.
 

Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wanahabari wameomba kuachi wa huru kwa wahariri wa magazeti manne ya Le Monde,Le reseau, le Mo nitor et le Future, waliokamatwa na kuwekwa rumande mwishoni mwa mwezi Aprili kufuatia agizo la Spika wa bunge la taifa hilo jijini Kinshasa.
 

Spika wa Bunge Aubin Minaku aliamuru polisi kuwashikilia wahariri hao baada ya kusema kuwa vyombo vyao vilimdhalilisha kwa kusema kuwa bunge lake ni kaburi na kwamba ni tapeli.
 

Wanahabari hao jijini Kinshasa wameomba kuachiwa huru kwa wahariri hao, bila ya masharti yoyote.
 

Mkuu wa taasisi inayochunguza vyombo vya Habari nchini DR Congo Polydor Muboyayi,amesema wamekuwa na mazungumzo na spika na kwamba walikubaliana kuwa wahariri hao watasikilizwa na kamati tendaji ya waandishi wa Habari wa DRC.
 

Nchini Burundi waandishi wa habari wanafanya maandamano kupinga kukandamizwa kwa uhuru wa vyombo vya habari ikiwemo muswada mpya wa sheria ambao ulipitishwa na bunge hivi karibuni.

Nchini Tanzania kunafanyika kongamano kubwa la uhjuru wa vyombo vya Habari lililoandaliwa na wadau mbalimbali wakiwemo MISA-TAN, Baraza la Habari Tanzania-MCT, Mfuko wa Vyombo vya Habari, Wamiliki wa Vyombo vya Habari-MOAT  na Jukwaa la Wahariri.

Kongamano hili linajadili pamoja na mambo mengine usalama wa waandishi wa habari na mazingira yao ya kazi.