SOMALIA-UINGEREZA

Rais wa Somalia Sheikh Mohamud aiomba Jumuiya ya Kimataifa kuisaidia nchi yake ili ijijenga upya baada ya vita vya zaidi ya miongo miwili

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron kwenye mkutano unaofanyika London
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron kwenye mkutano unaofanyika London

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amesema taifa hilo haliwezi kuendelea iwapo halitaungwa mkono vya kutoshja na Jumuiya ya Kimataifa kipindi hiki wakianza kujijenga upya baada ya kupitia vita vya zaidi ya miongo miwili. Sheikh Mohamud ametoa kauli hiyo kwenye mkutano unaozileta pamoja nchini hamisni sambamba na Mashirika yasiyo ya kiserikali unaofanyika nchini Uingereza ukiwa na lengo la kuisaida nchi hiyo kujijenga pamoja na kuwa na Jeshi lake imara.

Matangazo ya kibiashara

Rais Sheikh Mohamud amesema msaada pekee ambao wanautegemea kwa sasa ni kutoka Jumuiya ya Kimataifa inayoweza kusadia pakubwa juhudi zao za kuhakikisha nchi hiyo inasimama upya kiuchumi na kiusalama.

Kiongozi huyo amesema wamefanikiwa kufanya mabadiliko yakiwemo ya kuunda Bunge mpya pamoja na kuwa na katiba mpya lakini hawataweza kupiga hatua ya haraka iwapo watakosa kushikwa mkono na Jumuiya ya Kimataifa.

Mwenyeji wa Mkutano huo unaofanyika Jiji London ambaye ni Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ametoa onyo kwa washiriki na kuwaeleza iwapo hatua hazitachukuliwa Somalia inaweza ikawa chanzo cha vitendo vya ugaidi.

Cameron amesema Somalia inapaswa kusaidiwa kwa hali na mala hatraka iwezekanavyo kwani kwa kushindwa kufanya hivyo usalama wa duniani itakuwa matatani sababu kuna makundi hatari yanayoweza kutengenezwa katika taifa hilo.

Kiongozi huyo amesema usalama na kuimarika kwa utulivu katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika kutasaidia sana kuwepo kwa hali ya usalama katika eneo zima hilo ambalo kwa miaka zaidi ya ishirini imeshuhudia umwagaji wa damu.

Cameron amewazodoa wale ambao wanasema hawawezi kuisaidia Somalia kwa sasa na kuwaeleza ipo siku moja watakuwa wakwanza kujutia kwa kushindwa kuchukua hatua madhubuti mapema kama ambavyo inahitajika.

Mkutano huu umehudhuriwa na ujumbe kutoka Umoja wa Mataifa UN, Umoja wa Afrika AU, Shirika la Fedha la Kimataifa IMF pamoja na Mashirika mengine kutoka nchi jirani na Somalia.

Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta ni miongoni mwa viongozi wanaohudhuria Mkutano huo ambapo nchi yake ni miongoni mwa sehemu mwa Jeshi la Umoja wa Afrika AMOSIM lililofanikisha kuangushwa kwa ngome za Al Shabab.