BANGLADESH

Watu wanane wamepoteza maisha nchini Bangladesh baada ya moto kuzuka kwenye kiwanda cha nguo

Watu wanane wamepoteza maisha nchini Bangladesh baada ya kuzuka kwa moto kwenye kiwanda cha nguo ikiwa ni ajalia nyingine kwenye sekta hiyo ya viwanda kipindi hiki idadi ya watu waliokufa kwenye jengo la ghorofa ikifikia zaidi ya mia tisa.

Kiwanda cha nguo nchini Bangladesh kikishika moto na kusababisha vifo vya watu wanane
Kiwanda cha nguo nchini Bangladesh kikishika moto na kusababisha vifo vya watu wanane
Matangazo ya kibiashara

Watu hao wamefikwa na mauti baada ya kuteketezwa na moto huku wangine wakipoteza maisha baada ya kuwa katika harakati za kujiokoa kutoka ghorofa la tatu ambalo kiwanda hicho kinapatikana.

Mamlaka nchini Bangladesh zinaendelea kuhaha kuhakikisha zinajua chanzo cha kuzuka kwa moto huo ambao taarifa za awali zinasema ulizuka usiku kwenye kiwanda hicho kilichopo ghorofa la tatu katika jengo lenye ghorofa kumi na moja.

Jesho hilo la ghorofa kumi na moja lina viwanda viwanda viwili vya nguo katika Wilaya ya Darussalam na taarifa zinasema mmiliki wa kiwanda hicho cha Tung Hai kinachotengeneza maseta ni miongoni mwa waaathirika.

Mkurugenzi wa Uratibu wa kiwanda hicho Mahbubur Rahman amesema moto mkubwa ulizuka na kuendelea katika eneo kubwa la kiwanda lakini wakafanikiwa kuudhibiti baada ya muda.

Taarifa zinaeleza kuwa watu wamepoteza maisha kwenye ajali hiyo ya moto kutokana na kukosa hewa baada ya moshi mkubwa mwezi kutanda katika eneo kubwa la kiwanda huku wafanyakazi wamkishindwa kutoka kirahisi.

Katika hatua nyingine miili zaidi ya mia moja imepatikana kwenye mabaki ya jengo la ghorofa nane lililoanguka na kusababisha idadi ya watu waliopoteza maisha kwenye kiwanda hicho cha nguo kufikia mia tisa kumi na wawili.

Jengo la ghorofa nane lilianguka huku wafanyakazi wapatao elfu tatu wakiwa kazini ambapo hali ya hofu imeendelea kutanda kutokana na wengi kuhofia maiti zaidi zinaweza zikapatikana kwenye mabaki ya kifusi.

Kiongozi wa zoezi la uokozi Brigedia Jenerali Siddiqul Alam Sikder amesema wataendelea kusaka miili zaidi kwa kufukua vifusi kwa kuwa eneo hilo limetawaliwa na harufu kali inaashiria bado kuna miili imenaswa.