MALI-UFARANSA-NIGER

Mali yaomba ufadhili Umoja wa Ulaya

Raisi wa Ufaransa François Hollande sambamba na Raisi wa Niger Mahamadou Issoufou.
Raisi wa Ufaransa François Hollande sambamba na Raisi wa Niger Mahamadou Issoufou. REUTERS/Gonzalo Fuentes

Nchi ya Mali imeomba kwa wafadhili wa kimataifa hususan umoja wa ulaya EU takribani yuro bilioni 2.6 kusaidia kujenga upya nchi na kujaribu kuzuia kurejea kwa wapiganaji waasi ambao walifukuzwa katika miji mikubwa ya kaskazini.

Matangazo ya kibiashara

Ombi rasmi la fedha lilitolewa Ijumaa sanjari na tangazo la Rais wa Ufaransa Francois Hollande na mwenzake wa Niger ,Mahamadou Issoufou, kushinikiza uchaguzi wa kitaifa nchini humo kukamilika mwisho wa mwezi Julai.

Kulingana na waraka ulioandaliwa kwa ajili ya mkutano, utakaofanyika mjini Brussels siku ya Jumatano, Serikali ya Mali ilisema inaweza tu kuongeza kiasi kidogo cha pesa katika nusu ya bajeti iliyopendekezwa dola za marekani bilioni 5.6 kwa ajili ya maboresho mwaka 2013 na 2014.
 

Nchi ya Mali imekuwa katika harakati za kupambana na waasi wa kiislamu ambao walichangia kukosekana kwa usalama nchini humo hususan katika eneo la kaskazini.