SYRIA-MAREKANI-URUSI-UTURUKI

Uturuki yathibitisha Syria kutumia silaha za kemikali

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema anavithibitisho kwamba majeshi ya serikali ya Syria yanatumia silaha zenye kemikali dhidi ya majeshi ya upinzani.

Waziri mkuu wa Uturuki Tayyip Erdogan,amethibitisha Syria kutumia silaha za kemikali dhidi ya wapinzani
Waziri mkuu wa Uturuki Tayyip Erdogan,amethibitisha Syria kutumia silaha za kemikali dhidi ya wapinzani REUTERS/Umit Bektas
Matangazo ya kibiashara

Waziri huyo wa Uturuki amewaambia waandishi wa habari nchini Marekani akitaja ugunduzi wa mabaki ya makombora na baadhi ya majeruhi wa milipuko wakiwa na majeraha yenye viashiria vya kuathiriwa na silaha zenye kemikali.

Naye waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry amesema kuwa mpaka sasa kwa ushahidi huo mkubwa anaamini majeshi ya Syria yanatumia kemikali katika silaha.

Hapo awali ikulu ya Marekani ilikuwa na asilimia kadhaa za kuamini Syria ilitumia silaha za kemikali.

Mnamo mwezi uliopita raisi Barack Obama wa marekani alionya hatua ya matumizi ya silaha za kemikali kwa kukuita ni kuvuka mstari mwekundu.