SYRIA

Umoja wa mataifa na Urusi kuitisha mkutano wa haraka kuhusu Syria

Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akiwa na waziri wa mambo ya Kigeni wa Urusi Sergei Lavrov
Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akiwa na waziri wa mambo ya Kigeni wa Urusi Sergei Lavrov vivalanka.com

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon na Urusi zimekubaliana kwamba mkutano wa amani kuhusu Syria lazima ufanyike haraka iwezekanavyo hata kama Urusi inapinga shinikizo la dunia kwamba inawapa silaha wanajeshi wa serikali ya Damascus. 

Matangazo ya kibiashara

Ban amekutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov kabla ya mazungumzo ya baadaye leo Ijumaa na Rais wa Urusi Vladimir Putin kuhusu mkutano wa haraka wa kimataifa kuhusu Syria ambao lazima uhusishe wawakilishi wa pande mbili zinazopigana kwa mara ya kwanza.

Aidha Ban amewaambia waandishi wa habari kuwa matarajio yapo juu na mkutano lazima ufanyike haraka iwezekanavyo ambapo Lavrov amesisitiza kuwa kufanyika haraka kwa mkutano huo ni bora zaidi.

Hata hivyo Lavrov ametahadharisjha kuwa ni mapema sana kutaja tarehe ya mazungumzo ya Geneva ambayo kwa sasa yanatarajiwa kufanyika katika nusu ya kwanza ya mwezi wa sita kwa sababu uwasilishwaji halisi wa wajumbe wa Syria bado haujaamuliwa.

Mazungumzo haya mapya yanalenga kuwaleta pamoja waasi na wajumbe wa serikali husisha ni maana ya ni pamoja na wawili waasi fihatua ambayo ni ngumu ikizingatiwa kwamba baadhi ya wajumbe wa upinzani wamegoma kumtambua Assad kama sehemu ya mazungumzo.