MAREKANI

Ajali ya treni yajeruhi 60 Marekani

Treni mbili za abiria baada ya kugongana
Treni mbili za abiria baada ya kugongana www.cbsnews.com

Watu sitini wamejeruhiwa watano kati yao wanahalimbaya baada ya treni za abiria kugongana katika kitongoji cha Kaskazini mwa jiji la New York nchini Marekani. 

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa shirika la treni hiyo ya abiria amesema tukio hilo limehusisha treni iliyokuwa ikielekea katikati mwa jiji huku nyingine ikiwa katika uelekeo tofauti kwenda New Haven, katika jimbo la Connecticut.

Aidha shirika la Metro linalomiliki treni hizo ambazo husafirisha abiria wapatao laki mbili na elfu themanini kila siku limesema kuwa bado halijabaini chanzo cha ajali hiyo