Afghanistani

Askari 11 wa Afghanistan wauwawa kwa bomu

Moto ukiwaka baada ya kulipuka bomu
Moto ukiwaka baada ya kulipuka bomu gurdian.co.uk

Askari 11 wa Afghanistani wameuwawa Magharibi mwa Afghanistan baada ya bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara kulipuka leo Jumanne pamoja na mapigano Kusini mwa eneo hilo tete maafisa wamearifu. 

Matangazo ya kibiashara

Bomu hilo limeua askari walinzi sita katika jimbo la Herat leo Jumanne walipokuwa wakisafiri kuelekea katika bwawa la kuzalisha umeme ambalo linalindwa dhidi ya mashambulizi ya waasi.

Maafisa waliouwawa wanatoka katika Jeshi la kulinda wananchi la Afghanistan wa Umma,jeshi linaloendeshwa na serikali ambalo linatoa ulinzi kwa misafara ya kimataifa ya usalama , vikundi vya misaada na maeneo ya ujenzi yanayo fadhiliwa na mataifa ya kigeni.

Mlipuko umerindima ukitokea garini ambako wakati watu hao wakielekea katika wilaya ya Obe huko Herat ambako India inajenga upya bwawa la kuzalisha umeme.

Hata hivyo hakuna madai ya kundi lolote kuhusika na shambulizi hilo ingawa mabomu ya aina hiyo mara nyingi yanahusishwa kutekelezwa na kundi la Taliban, kundi kubwa la wapiganaji ambalo limekuwa likifanya uasi dhidi ya serikali ya mjini Kabul.