Israel-Syria

Israel yajibu mashambulizi ya vikosi vya jeshi la Syria

Kikosi cha IDF kikijibu mashambulizi
Kikosi cha IDF kikijibu mashambulizi timesofisrael.com

Askari wa Israel wanaofanya doria kwenye eneo lenye mgogoro la milima ya Golani mpakani na Syria wamefanya mashambulizi ya malipizi baada ya kushambuliwa usiku wa manane,Taarifa ya vikosi vya usalama vya Israel vimesema. 

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi ya usiku yalielekezwa katika kikosi doria cha IDF kilichokuwa mpakani katikati mwa vilima vya Golani , na kuharibu gari la jeshi taarifa ya jeshi imearifu na kuongeza kuwa hakuna yeyote aliyejeruhiwa.

Kwa kujibu mashambulizi vikosi vya IDF vilirusha risasi kuelekea yalikotokea mashambulizi dhidi yao ambapo hata hivyo IDF inalitazama tukio hilo kwa masikitiko na tayari kimepeleka malalamiko yake katika kikosi cha umoja wa mataifa cha kuzuia mapigano UNDOF ambacho kinafanya doria katika eneo hilo.

Mapema Jumatatu, jeshi limearifu kwamba silaha ndogo za risasi zilizorushwa kutoka Syria zimerushwa katika vilima vya Golan usiku wa kuamkia leo bila kusababisha madhara.