KENYA-MAREKANI

Marekani yasema inashirikiana na mataifa yote ya Afrika ikiwemo Kenya

Raisi wa Marekani Barack Obama,anataraji kuanza ziara barani Afrika mnamo mwezi June.
Raisi wa Marekani Barack Obama,anataraji kuanza ziara barani Afrika mnamo mwezi June. AFP

Serikali ya Marekani imesisitiza kuwa ingali na ushirikiano wa karibu na mataifa yote ya bara Afrika ikiwemo Kenya, baada ya madai kuzuka kuwa Marekani huenda inajitenga na Kenya baada ya Washington kutangaza kuwa rais obama atazuru mataifa matatu ya bara Afrika, huku Kenya ikikosa kujumuishwa.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Msemaji wa serikali ya Kenya Muthui Kariuki amewaambia waandishi wa habari kuwa, nchi ya Marekani kama nchi nyingine ina uhuru wa kuamua mambo yake na rais Obama ana haki ya kutembelea nchi anayoichagua.

Wadadisi wa masuala ya siasa za kimataifa wameiongelea kuhusu ziara ya rais Obama barani Afrika na kutotembelea nchi ya kenya kuwa ni mbinu ya kiongozi wa Marekani kukwepa kujihusisha na taifa hilo kutokana na mashtaka yanayowakabili viongozi wa Kenya.

Serikali ya Washington ilitangaza kuwa rais Obama atazuru mataifa matatu ya bara Afrika katika ziara yake mwezi June, huku Kenya ikikosa kujumuishwajambo lililozua hoja na madai mbalimbali.