Tume ya ukweli haki na maridhiano yatoa ripoti ya ukiukwaji wa haki za binadamu kenya kuanzia uhuru.
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wametajwa kuhusika katika vurugu za baada za uchaguzi katika ripoti iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na gamu inayochunguza ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Kenya kuanzia Uhuru wa taifa hilo 1963.
Imechapishwa:
Kwa niaba ya watu walioathirika na matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu tume ya ukweli na maridhiano imependekeza viongozi hao kuomba radhi kwa Wakenya.
Hata hivyo madai hayo ya tume yamepingwa na raisi Kenyatta na naibu wake.
Tume ya ukweli haki na maridhiano iliundwa kufuatia machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu miaka mitano iliyopita kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Kenya.
Katika vurugu za baada ya uchaguzi takribani watu elfu moja mia tano walipoteza maisha na wengine laki sita wakilazimika kuyahama makazi yao.