MAREKANI

Zoezi la uokozi Marekani lakamilika,matumaini ya kuwapata manusura zaidi yatoweka

Jitihada za Vikosi vya uokoaji vinaendelea na kazi ya kusafisha mji wa Oklahoma nchini Marekani huku matumaini ya kuwapata watu wengine wakiwa hai yakitoweka kutokana na kukamilika kwa sehemu kubwa ya zoezi la uokoaji.

Baadhi ya waokoaji,polisi na mashuhuda wakiwa katika moja ya eneo lililoathiriwa na kimbunga cha Tornado ambacho kimesababisha vifo huko Moore,Oklahoma nchini Marekani
Baadhi ya waokoaji,polisi na mashuhuda wakiwa katika moja ya eneo lililoathiriwa na kimbunga cha Tornado ambacho kimesababisha vifo huko Moore,Oklahoma nchini Marekani REUTERS/Gene Blevins
Matangazo ya kibiashara

Polisi wamearifu jitihada za uokozi zilikabiliwa na changamoto mbalimbali siku ya jumanne ingawa takribani watu mia moja wamepatikana hai.

Hata hivyo Rais wa Marekani Barack Obama ameahidi serikali yake kuhakikisha inatoa msaada wa hali na mali kwa mamia ya familia ambazo zimepoteza makazi na ndugu zao kufuatia kimbunga cha Tornado kilichokumba eneo la Moore kwenye mji wa Oklahoma.

Rais Obama amewataka raia wa Marekani kuungana kuwasaidia wananchi walioathiriwa na kimbunga hicho ambapo alitangaza hali ya dharura kwenye mji wa Moore kutokana na kushuhudiwa madhara makubwa yaliyotokana na kimbunga hicho.

Watu zaidi ya 24 wameripotiwa kupoteza maisha wengi wakiwa watoto waliokuwa shuleni wakati kimbunga hicho kikitokea.