Waziri Cameron na wakuu wa usalama London wajadili tukio la kigaidi
Wakuu wa usalama nchini Uingereza wamefanya mkutano kujadili mauaji ya kikatili dhidi ya mwanajeshi wa Uingereza,ambayo yalitekelezwa na Watu wawili wanaodaiwa kuwa ni waislamu wenye msimamo mkali,ambao kwa sasa wanashikiliwa na polisi mjini London Uingereza.
Imechapishwa:
Picha za video zimewaonesha watuhumiwa wakiwa na mapanga waliotumia kumkatakata mwanajeshi huyo na kisha kumtelekeza barabarani huku wakisikia wakitamka maeneo ya kulipiza kisasi dhidi ya ukatili wanaotendewa ndugu zao.
Mtu aliyeuawa kikatili amethibitishwa kuwa alikuwa mwanajeshi na tayari familia yake imearifiwa kuhusu kifo chake.
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amelaani mauaji hayo na kusema kuwa kuna vithibitisho tosha kuwa tukio hilo ni la kigaidi halitavumilika.