UINGEREZA-MASHARIKI YA KATI-

Waziri Hague aipa kipaumbele amani ya mashariki ya kati

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza William Hague amesema kuwa suala la amani kati ya israel na palestina linapewa kipaumbele wakati huu ambapo a,ekutana na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza,William Hague
Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza,William Hague REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kabla ya kukutana na Netanyahu, waziri Hague aliwaambia waandishi wa habari ''Mchakato wa amani ya mashariki ya kati ni suala la msingi kwa Uingereza na ulimwengu kwa ujumla.

Kiongozi huyo aliongeza kuwa mataifa hayo yanakaribia makubaliano makubwa ya kufufua mazungumzo ya amani yaliyooneshwa na raisi wa Marekani katika ziara yake ya hivi karibuni na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry.

Ziara ya Hague ni jitihada za kuwataka pande zote mbili kuendeleza mchakato mbele wa kiuongozi ambao utakuwa na manufaa na kusisitizwa kuwa amani ni ya lazima na ni muhimu kupatikana.

Waziri wa mambo ya kigeni wa marekani John Kerry alikuwa Jerusalem alhamisi katika ziara yake ya nne nchini humo tangu alipokabidhiwa wadhifa huo mnamo mwezi February,wa kuhimiza kurejewa kwa mchakato wa amani ambayo ilitoweka mnamo mwezi Septemba 2010.

John Kerry amekutana na viongozi wa palestina huko Ramallah wakati waziri Hague akisubiriwa kuhutubia na kukutana na kiongozi wa Palestina Mahmud Abbas.