DR Congo-Umoja wa mataifa UN

Raia DR Congo watumaini kurejea kwa amani

Katibu mkuu Ban Ki-moon,Raisi wa DRC  Joseph Kabila na Raisi wa Benki ya dunia Jim Yong Kim wakiwa Kinshasa, le 22 mai 2013.
Katibu mkuu Ban Ki-moon,Raisi wa DRC Joseph Kabila na Raisi wa Benki ya dunia Jim Yong Kim wakiwa Kinshasa, le 22 mai 2013. AFP/Junior D.Kannah

Raia wa mashariki mwa nchi ya jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwenye mji wa Goma wameeleza matumaini yao ya kushuhudiwa kurejea kwa amani hivi karibuni kwenye eneo hilo pindi vikosi vya Umoja wa Mataifa vitakapowasili kukabiliana na waasi wa M23.

Matangazo ya kibiashara

Kauli hizo zimetolewa saa chache baada ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kumaliza ziara yake mashariki mwa nchi hiyo ambapo ameahidi kuanza kazi kwa operesheni ya wanajeshi maalumu wa umoja huo ndani ya mwezi mmoja ujao.

Katibu mkuu Ban ameyasema hayo wakati akihitimisha ziara yake kwenye mji wa GOMA alhamisi ambapo amejionea hali ya usalama na hali ya raia ambao wamekuwa wakitaabika kutokana na mapigano kati ya waasi wa M23 na vikosi va serikali vya FRDC.

Katika ziara hiyo, Ban aliambatana na mkuu wa benki ya Dunia, Jim Yong Kim ambaye alitangaza msaada zaidi kwa nchi ya jamhuri ya kidemokrasia ya kongo DRC.

Hata hivyo mkuu wa tume ya usalama wa Umoja wa Afrika, Ramtane Lamamra anasema kuwa vita pekee haitatatua mzozo wa DRC badala yake hata malalamiko ya M23 ni lazima yafikiriwe.

Wakati wa ziara ya Ban kuliripotiwa makabiliano ya risasi kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa serikali kwenye baadhi ya maeneo jirani na alipokuwa katibu mkuu Ban.

Tayari wakuu hao wamewasili mjini Kigali Rwanda alhamisi jioni na wamekuwa na mazungumzo na rais wa Rwanda Paul Kagame ambapo baadae ijumaa wataelekea mjini Kampala Uganda kwa mazungumzo na rais Yoweri Museveni.