SYRIA-URUSI-UINGEREZA

Upinzani waitaka serikali ya Assad kuthibitisha kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa kutatua mzozo wa syria

Upinzani nchini Syria umeitaka serikali ya raisi Assad kutangaza kama itahudhuria mkutano wa kimataifa wa kuisaka suluhu baada ya Urusi kudai serilaki hiyo imekubali kwa masharti kuhudhuria mkutano huo.

Askari watiifu wa serikali ya raisi Bashar Al Assad wakiwa katika moja ya operesheni zao kupambana na wapinzanimai 2013.
Askari watiifu wa serikali ya raisi Bashar Al Assad wakiwa katika moja ya operesheni zao kupambana na wapinzanimai 2013. AFP PHOTO/JOSEPH EID
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa muungano wa taifa Louay Safi, amezungumza na mkutano wa upinzani wa syria huko Istanbul kuwa muungano huo unetaka kusikia kauli ya kukubali kuhudhuria kitangazwa na serikali ya raisi Assad.

Upinzani umedai kuwa unahitaji ufafanuzi zaidi kwakuwa tangazo hilo bado linautata na kushangazwa kwanini serikali ya Damascus isiarifu.

Mkutano wa kimataifa unatarajiwa kufanyika mnamo tarehe 2 ya june ambapo umelenga kumaliza vita vya syria vilivyodumu kwa miaka miwili sasa na kupoteza maisha ya watu elfu tisini sasa.

Waandaaji wa mkutano huo wametakiwa kuhakikisha pande mbili zinazohasimiana nchini Syria zinashiriki mkutano huo.

Mkutano wa kimataifa ulipendekezwa na Urusi mshirika muhimu wa serikali ya Assad na Marekani ambayo inaunga mkono upinzani kupambana kuuondoa utawala wa raisi Assad.

Mapema ijumaa msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni nchini Urusi Alexander Lukashevich aliarifu kuwa serikali ya Moscow imepokea makubaliano yenye masharti ili Dascus kushiriki mkutano huo.