Watuhumiwa wawili washikiliwa na polisi Uingereza wakihusishwa na mauaji ya mwanajeshi
Polisi nchini Uingereza wamefanikiwa kuwakamata washukiwa wengine wawili zaidi kuhusiana na tukio la kushambuliwa na kuuawa kikatili kwa mwanajeshi wake mjini London ambapo makachero wa Uingereza wamesema kuwa washukiwa hao wana umri kati ya miaka 28 na 22 wenye asili ya Nigeria bila ya kutaja majina yao kwasababu za kiusalama.
Imechapishwa:
Siku ya alhamisi waziri mkuu David Cameron alifanya mkutano wa dharura na kamati ya usalama na kuagiza kufanyika uchunguzi wa kina huku akiapa nchi yake kutovumilia vitendo vya kigaidi nchini humo.
Serikali ya Uingereza imemtaja mwanajeshi aliyeuawa kuwa ni Lee Rigby ambapo sasa ulinzi wa zaidi ya askari 1200 umewekwa mjini London.
Serikali ya Uingereza imekiri bado ipo thabiti kukabiliana na mashambulizi yoyote ambayo yanapangwa huku watuhumiwa wawili ambao wanatajwa kuwa ni Waislam wenye Msimamo Mkali wameshamakatwa baada ya kutekeleza mauaji ya kumkatakata kwa panga mwanajeshi huyo wa Uingereza.
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amesema lililofanyika ni ishara tu ya kuusaliti Uislam na serikali inalichukua tukio hilo kuwa la kigaidi na wataendelea kupambana na matukio kama hayo.
Baraza la Waislam nchini Uingereza nalo limelaani vikali mauaji hayo yaliyofanywa na mtu aliyetamka Allah Akbar kama ilivyoelezwa Katibu Mkuu wake Faruk Murad.
Meya wa Jiji la London Boris Johnson naye akaeleza Mauji hayo ya mwanajeshi wa Uingereza yaliyofanywa na vijana wawili yamewashtua wengi nchini humo.
Shambulizi hili limezua maswali mengi uhusiano uliopo baina ya Uingereza na Waislam duniani huku wengine wakitaka hatua zaidi zichukuliwe kukabiliana na vitendo vya kigaidi katika Taifa hilo.