SYRIA

Ushiriki wa Syria katika mkutano wa kimataifa wa kusaka amani wazua wasiwasi

Rais wa Syria Bashar ala Assad
Rais wa Syria Bashar ala Assad aim.org

Kauli ya urusi kuwa serikali ya rais Bashar ala Assad imekubali kuhudhuria mkutano wa amani wa kimataifa juu ya mgogoro wa Syria imeweka maswali na wasiwasi miongoni mwa wapinzani waliogawanyika wa Rais Bashar al-Assad. 

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa Urusi Alexander Lukashevich jana Ijumaa alisema kuwa waliwamepokea hakikisho la serikali ya Damascus kuwa ingehudhuria na kushiriki katika mazungumzo, wakati alipotembelewa wiki hii na Naibu Waziri mambo ya kigeni wa Syria Faisal Muqdad.

Juhudi za Kidiplomasia za kuitisha mkutano wa kwanza uliopendekezwa na Urusi na Marekani Mei 7 zimepata nguvu mpya baada ya waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry na mshirika wake wa Urusi Sergei Lavrov kukubaliana kwa njia ya simu kukutana mjini Paris siku ya Jumatatu kujadili hatua za kuwezesha pande zote za mzozo kushiriki mazungumzo hayo.