COLOMBIA-FARC

Waasi wa FARC na Serikali ya Colombia wafikia suluhu kuhusu mgawanyo wa ardhi

Serikali ya Colombia na kundi la waasi wa FARC hatimaye wamefikia makubaliano kuhusu suala la ardhi ambalo lilikuwa ajenda kuu ya mazungumzo ya kusaka suluhu ya mapigano yaliyodumu kwa zaidi ya miongo mitano.

Viongozi wa Serikali ya Colombia na waasi wa FARC wakiwa kwenye mazungumzo mjini Havana, Cuba
Viongozi wa Serikali ya Colombia na waasi wa FARC wakiwa kwenye mazungumzo mjini Havana, Cuba Reuters
Matangazo ya kibiashara

Makubaliano kati ya Serikali ya Bogota na waasi wa The Revolutionary Armed Forces of Colombia FARC yatashuhudia wananchi waliopoteza ardhi yao wakirejeshewa maeneo yao na wale ambao hawana makazi wakipewa makazi mapya.

Balozi wa Cuba, Carlos Fernandez de Cossio ambaye anashiriki kwenye mazungumzo hayo amesema kwa sasa mazungumzo yamelenga kumaliza mzozo wa ardhi ambao umekuwa kikwazo kwenye mazungumzo hayo na kwamba sasa suluhu imepatikana kwa kukubaliana kwenye mamabo muhimu kuhusu ardhi.

Waasi wa kundi la FARC wanataka kupatiwa sehemu ya ardhi kwenye maeneo ambayo wanayamiliki na kwamba wapiganaji wake warejeshewe ardhi ambayo imechukuliwa na Serikali na kwamba wale ambao hawana makazi wapewe ardhi kuiendeleza.

Makubaliano haya ni muhimu kwa pande hizo mbili kufuatia mazungumzo yaliyodumu kwa zaidi ya miezi sita mjini Havana Cuba ambapo jaenda ya kwanza na kuu ilikuwa ni mgawanyo wa ardhi.

Makubaliano hayo yamepokelewa kwa shangwe mjini Bogota na kwa upande wa waasi wa FARC ambao wanaamini suala la ardhi ndilo lilikuwa jambi la msingi wa mazungumzo hayo kumaliza mzozo wao.

The step, the first major advance in six months of peace talks in Havana, was widely celebrated -- but it is part of a larger package still being bargained.