NIGER-CHAD

Niger yaionya Chad dhidi ya mashambulizi ya kigaidi

Reuters

Rais wa Niger ameionya nchi ya Chad dhidi ya mashambulizi kama yaliyotekelezwa kwenye mgodi wake unaomilikiwa na kampuni ya Ufaransa kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ambapo watu zaidi ya 20 waliawa.

Matangazo ya kibiashara

Rais Mahamadou Issoufou amesema kuwa maofisa usalama wa nchi yake wamebaini mpango uliopo wa kutekelezwa kwa shambulio nchini Chad ikiwa ni mfululizo wa mashambulizi yaliyopangwa na makundi ya kigaidi kwenye nchi hizo.

Ameongeza kuwa wapiganaji waliotekeleza shambulio la juma lililopita, walitokea kusini mwa moaka wake na nchi ya Libya na kwamba huenda wapiganaji hao wamepaanga kushambuli nchi ya Chad.

Nchi ya Niger na Chad ni miongoni mwa mataifa ambayo yalipeleka wanajeshi wake nchini Mali ambapo shambulio la hivi karibuni lililenga maslahi ya taifa la Ufaransa pamoja na nchi husika kwa ushiriki wake nchini Mali.

Kundi la MNLA lenye ushirikiano na mtandao wa kigaidi duniani wa Al-Qaeda lilikiri kuhusika na shambulio hilo na kuapa kuendelea kutekeleza mashambulizi zaidi dhidi ya Serikali na maslahi ya Ufaransa.

Hata hivyo licha ya kuonya kutekelezwa kwa shambulio hilo, rais Issoufou hakuweka wazi iwapo wamewakamata watu ama kubaini hasa ni lini wapiganaji hao watatekeleza shambulio hilo.