Polisi nchini Uingereza wamkamata mtuhumiwa wa 10 kuhisiana na mauaji ya mwanajeshi wake
Polisi nchini Uingereza wanaendelea na msako wa watu zaidi ambao wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya mwanajeshi wake aliyeuawa juma moja lililopita kwa kukatwakatwa na panga.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Polisi wamemkamta mtu mwingine zaidi kuhusiana na tukio hilo na kufanya idadi ya waliokamatwa mpaka sasa kuhusiana na tukio hilo kufikia watu kumi ambao wanaendelea kuhojiwa na polisi kuhusu uhusika wao.
Idadi hiyo inawajumuisha washtakiwa wawili wa kutekeleza mauaji hayo, Michael Adebolajo na Michael Adebowale ambao kwa pamoja walitekelza shambulio hilo nje ya kambi moja ya jeshi kwenye eneo la Woolwich mjini London.
Katika hatua nyingine watu wanakadiriwa kufikia elfu moja wameandamana nje ya ofisi ya waziri mkuu David Cameron wakishinikiza achukue hatua zaidi dhidi ya makundi ya watu wenye msimamo mkali nchini humo.
Kufuatia tukio hilo, waziri mkuu Cameron ametangaza kuunda kikosi kazi cha kupambana makundi ya watu wenye msimamo na kwamba kitahusika na kukabiliana na vikundi vyote ambayo vinamisimamo mkali.
Serikali ya Uingereza imejikuta kwenye shinikizo kubwa baada ya tukio hilo kufuatia kukiri kuwa mtuhumiwa wa mauaji hayo alitakiwa kufanya kazi na maofisa usalama wa MI5 na pia aliwahi kukamatwa nchini Kenya akihusishwa kuwa na uhusiano na kundi la wanamgambo wa Al-Shabab.