MALI-ECOWAS

Rais wa Burkina Faso yuko nchini Mali kwa mazungumzo, upinzani wakosoa msimamo wa Serikali ya Ufaransa

Rais wa Burkina Faso, Blaise Compaore ambaye ni msuluhishi mkuu wa mzozo wa Mali ameanza mazungumzo na viongozi wa Serikali na wale wa waasi wa Tuareg kujaribu kutafuta suluhu kupisha uchaguzi mkuu.

Rais wa Burkina Faso, Blaise Compaore
Rais wa Burkina Faso, Blaise Compaore Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo yanafanyika wakati huu ambapo kumezuka hofu ya kuharibika kwa zoezi la uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi ujao ambapo kundi la waasi wa Tuareg na wale wa MNLA waliokubali kushirikiana na Serikali wanataka kuendelea kusalia kwenye miji wanayoshikilia wakiwa na utawala wao.

Jumuiya ya Maendeleo ya Kuichumi kwa nchi za Magharibi mwa Afrika ECOWAS imesema kuwa lengo lake ni kuhakikisha kuwa uchaguzi wa Mali unafanyika kwa huru na haki wakati huu ambapo bado kuna hali ya sintofahamu kaskazini mwa nchi hiyo.

Rais Compaore awali alikutana na Tiebile Drame mwakilishi wa Serikali ya Mali kaskazini mwa nchi hiyo ikiwa ni siku moja toka Serikali itangaze tarehe 28 ya mwezi huu kama tarehe rasmi ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu.

Nchi ya Mali inatarajiwa kufanya duru lake la kwanza la uchaguzi mkuu wa Urais mwezi July tarehe 28 ambapo mazungumzo hayo ni muhimu kwa mustakabali wa kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa huru na haki.

Mazungumzo hayo yanalenga kutiwa saini kwa makubaliano ya amani kati ya waasi na Serikali ili kuleta suluhu ya kisiasa nchini Mali.

Katika hatua nyingine upinzani nchini humo umekosoa vikali kauli ya rais wa Ufaransa, Francois Hollande kuhusu eneo la Kidal ambako wanajeshi wa Ufaransa wameapa kukaa huko mpaka pale hali ya usalama itakaporejea.

Upinzani unasema nchi ya Ufaransa inataka kufanya eneo la kaskazini mwa nchi hiyo kama mali yake na kuleta ukoloni mambo leo nchini humo.

"We have high hopes that we can move quickly towards the signing of an interim accord" enabling the election to be held throughout all Mali's territory, he added.