LIBYA

Spika wa bunge la Libya, al-Megaryef kujiuzulu nafasi yake

Mohamed al-Megaryef spika wa bunge la LIbya anayeondoka
Mohamed al-Megaryef spika wa bunge la LIbya anayeondoka Reuters

Spika wa bunge la nchini LIbya Mohamed al-Megaryef hii leo anatarajiwa kuachia nafasi yake kama kiongozi wa shughuli za bunge kufuatia sheria iliyopitishwa kuzua viongozi waliokuwa chini ya utawala wa marehemu kanali Gaddafi kushika ofisi.

Matangazo ya kibiashara

Bunge la nchi hiyo hivi karibuni lilipitisha sheria inayokataza viongozi waliokuwa chini ya utawala wa marehemu kanali Muamar Gaddafi kushika nafasi yoyote ya uongozi kufuatia maandamano ya wapiganaji waliozingira ofisi kadhaa kushinikiza kujiuzulu kwa viongozi hao.

Hivi karibuni baadhi ya wapiganaji wenye silaha walizingira ofisi za Serikali ambazo wanadai kulikuwa na viongozi waliokuwa chini ya utawala ulioangushwa na kushinikiza viongozi hai kujiuzuu nafasi zao.

Megaryef alichaguliwa kuwa spika wa bunge mwezi August mwaka 2012 ambapo wakati wa mapinduzi alikimbilia uhamishoni na kuongoza harakati za upinzani kupindua serikali ya kanali Gaddafi.

Wakati wa utawala wa Gadadafi, kiongozi huyu aliwahi kuhudumu kwenye ofisi mbalimbali ikiwemo kama balozi wa Libya nchini India miaka ya 80.

Megaryef alifanikiwa kushinda majaribio ya kuuawa mjini Rome mwaka 1981, mjini Casblanca mwaka 1984 na mjini Madrid mwaka 1985.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanaona kuwa kujiuzulu kwa kiongozi huyo kutakuwa pengo kwa utawala wa Libya kwakuwa haitakuwa na wasomi wengi na wenye uzoefu kungoza Serikali.