CHINA-IMF

IMF: Ukuaji wa uchumi wa China waendelea kusuasua

Uchumi wa China waelezwa kupungua kasi ya ukuaji wake kwamujibu wa ripoti ya IMF
Uchumi wa China waelezwa kupungua kasi ya ukuaji wake kwamujibu wa ripoti ya IMF Reuters

Shirika la fedha duniani IMF limesema ukuaji wa uchumi wa taifa la China umeshuka hadi kufikia asilimi 7.75 kwa mwaka 2013 ukilinganisha na mwaka uliopita ambapo ulikuwa kwa asilimia 8.0.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya ukuaji wa uchumi wa dunia ilitolewa na IMF mwezi mmoja uliopita imeonesha kuwa ukuaji wa uchumi wa China umeendelea kusalia kwenye kiwango cha awali na kwamba umeshuka kwa asilimia 1 ukilinganisha na vile ilivyotabiriwa kwa mwaka uliopita.

Hata hivyo ripoti hiyo imeongeza kuwa licha ya kushuka kwa pato ghafi la China, uchumi wake unatarajiwa kuanza kuimarika ifikapo katikati ya mwaka huu na mwaka ujao ambapo huenda ukakua kwa karibu asilimia 8.0 hadi 8.2.

Kaimu mkurugenzi wa shirika hilo amesema kuwa licha ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na China kwenye mataifa yanayoendelea lakini ukuaji mdogo wa biashara za nje ndio imetajwa kuwa sababu kubwa ya kuifanya nchi hiyo kushindwa kuimarika kiuchumi kama ilivyotabiriwa.

IMF imongeza kuwa ukuaji mdogo wa uchumi wa China haujawahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 13 licha ya taifa hilo kuendelea kuwa kinara kwenye ukuaji wa uchumi wa dunia kwa sasa.

Hivi karibuni nchi ya China ilitangaza kuongeza uzalishaji na kufanya biashara zaidi na mataifa ya Ulaya kwa lengo la kuzisaidia nchi wanachama wa Umoja huo kuimarika kiuchumi lakini kuisaidia China kusimamisha uchumi wake pia.