PAKISTAN-TALIBAN-MAREKANI

Kiongozi wa juu wa kundi la Taliban nchini Pakistan auawa kwenye shambulio la ndege zisizo na rubani

Waliur Rehman anayedaiwa kuuawa kwenye shambulio la ndege za Marekani
Waliur Rehman anayedaiwa kuuawa kwenye shambulio la ndege za Marekani Reuters

Shambulio lililotekelezwa na ndege za Marekani zisizo na rubani kwenye jimbo la Waziristan kaskazini mwa nchi ya Pakistan linadaiwa kumuua kiongozi wa pili wa nagzi za juu wa kudni la Taliban nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Watu sita wamedhibitishwa kuuawa kwenye shambulio hilo ambalo Marekani inasema lililenga wanamgambo wa Taliban waliokuwa wamejifisha kwenye milima ya Waziristana ambako wamekuwa wakipanga njama zao za kutekeleza mashambulizi ya kujitoa muhanga.

Waliur Rehman anatajwa na Serikali ya Marekani kama kiongozi wa pilis wa juu wa kundi la Taliban nchini Pakistan ambapo ilikuwa imetoa donge nono la dola milioni tano iwapo kungepatikana taarifa za alikojificha.

Rehman ambaye wakati fulani anatajwa kuwa msemaji wa kundi hilo nchini Pakistan amenusurika mara kadhaa kwenye mashambulizi ya Marekani akiwa na viongozi wengine wa kundi hilo.

Kundi la Taliban nchini Pakistan limekataa kudhibitisha iwapo kiongozi wao ameuawa kwenye shambulio hilo ingawa Pakistan yenyewe imedhibitisha kuwa ni miongoni mwa watu sita waliouawa.

Shambulio hilo linatekelezwa wakati huu ambapo nchi ya Marekani inaandaa mpango maalumu wa kutekeleza mashambulizi ya ndege zisizo na rubani mashambulizi ambayo katika siku za hivi karibuni yamekosolewa kutokana na kuua raia wasio na hatia.

Waziri mkuu Sharif ambaye ataapishwa juma lijalo tayari amekosoa operesheni za ndege hizo na kuongeza kuwa atapitia upya mpango huo wa Marekani kuendelea kutumia ndege hizo kufanya mashambulizi.