SYRIA-UTURUKI-URUSI

Upinzani nchini Syria wasema hautashiriki mazungumzo ya amani, wataka Hezbollah waondoke nchini humo kwanza

Upinzania nchini Syria umesema hautashiriki kwenye mazungumzo ya amani ya mjini Geneva yaliyopangwa kuanza mwezi jao iwapo nchi ya Iran itaendelea kuwafadhili wapiganaji wa Hezebollah kuusaidia utawala wa rais Bashar al-Assad.  

Rais wa mpito wa baraza la Syria, George Sabra
Rais wa mpito wa baraza la Syria, George Sabra Reuters
Matangazo ya kibiashara

"Baraza la muungano wa Syria halitashiriki mazungumzo ya kimataifa wala kushiriki juhudi zozote za kutafuta amani iwapo wapiganaji wa Hezbolla wataendelea na uvamizi wao nchini Syria". Amesema rais wa muda wa baraza hilo, George Sabra.

Akizungumza mjini Instanbull na waandishi wa habari, Sabra amesema kuwa baada ya kuketi kama baraza wamekubaliana kutojiingiza kwenye mazungumzo yaliyoandaliwa na Urusi na Marekani mwezi ujao iwapo Hezbollah haitaacha uvamizi wake nchini mwao.

Kiongozi huyo ameongeza kuwa uvamizi unaofanywa na Hezbollah kwa msaada wa Iran kwenye mji wa Quasary kunaendana kinyume na mkataba wa kimataifa wa kulinda raia na kwamba kundi hilo linakiuka haki za binadamu.

Wapoganaji wa Hezbollah wamekuwa wakipigana sambamba na wanajeshi wa Serikali ya Syria katika kukabiliana na waasi ambao kwa sehemu kubwa sasa wamekimbia mji huo na uko kwenye himaya ya wanajeshi wa Serikali.

Awali wanajeshi huru wa Syria walikuwa wameuteka uwanja wa ndege wa Quasary lakini walijikuta wakiuachia baada ya kuzidiwa nguvu na wapiganaji wa Hezbollah waliokuwa sambamba na vikosi vya Serikali.

Tayari serikali ya Urusi imeota tamko kuhusu msimamo wa waasi ambapo kupitia waziri wake wa mambo ya kigeni Sergei Lavrov amesema waasi wanaonesha kutotaka amani ya kudumu nchini Syria kwa kuendelea kutoa masharti ya kushiriki mazungumzo.

Urusi imelaani msimamo wa waasi na kuongeza kuwa kufanya hivyo kunaendana kinyume na juhudi ambazo jumuiya ya kimataifa imekuwa ikifanya katika kuwakutanisha waasi hao na upande wa Serikali.

Marekani kupitia ikulu yake imetoa taarifa kuwataka wapiganaji wa Hezbollah kuondoka ndani ya Syria kwa kile ilichodai kuwa wanakiuka mkataba wa kimataifa.