THE HAGUE-SERBIA

Mahakama ya Umoja wa Mataifa UN yawaachia huru washukiwa wawili wa mauaji ya vita vya Bosnia, 1990

Mmoja wa watuhumiwa walioachiliwa huru na mahakama ya Umoja wa mataifa kuhusiana na ushiriki wake wa vita vya Bosnia akipongezana na wakili wake baada ya hukumu
Mmoja wa watuhumiwa walioachiliwa huru na mahakama ya Umoja wa mataifa kuhusiana na ushiriki wake wa vita vya Bosnia akipongezana na wakili wake baada ya hukumu Reuters

Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya mjini The Hague Uholanzi, jana jioni imewafutia mashtaka ya mauaji yaliyokuwa yanawakabili maofisa wawili wa usalama wa Serbia wakati wa vita vya Bosnia mwaka 1990.

Matangazo ya kibiashara

Majaji kwenye mahakama hiyo wamesema kuwa waendesha mashtaka kwenye kesi hiyo hawakuwa na ushahidi wa kutosha kuweza kuwashawishi kuwatia hatiani maofisa hao wawili kutokana makosa waliyoshtakiwa nayo.

Uamuzi huo wa mahakama kuwafutia makosa Franko Simatovic na Jovica Stanisic umekuja kufuatia kesi hiyo iliyodumu kwa karibu miaka mitatu na uamuzi wake kusburiwa kwa hamu kubwa na wananchi wa Serbia.

Watuhumiwa hao wawili wote kwa pamoja walikuwa wanaidaiwa kuhusika na kuagiza wanajeshi wa Serikali kutekeleza mauaji dhidi ya raia Bosnia.

Wakati uamuzi huo ukitolewa washukiwa wote wawili walionesha kushtushwa na uamuzi wa mahakama kwakile kilichoelezwa kuwa hawakuamini iwapo mahakama hiyo imewakuta hawana hatia ya makosa yaliyokuwa yanawakabili.

Stanisic ambaye alikuwa mkuu wa kitengo maalumu cha makachero wa polisi na mtu wa pili wa karibu wa kiongozi wa Serbia wakati huo, Slobodan Milosevic.

Waziri mkuu wa Serbia, Ivica Dacic amepongeza uamuzi wa mahakama hiyo na kuongeza kuwa inadhihirisha utendaji kazi mzuri wa mahakama za ndani za serbia na ile ya Umoja wa Mataifa.