DRC

Nyaraka za kesi ya mwanaharakati, Florobert Chebeya zaibiwa ofisini kwa wakili wake

Mwanaharakati wa haki za binadamu nchini DRC aliyeuawa mwaka 2010, Floribert Chebeya
Mwanaharakati wa haki za binadamu nchini DRC aliyeuawa mwaka 2010, Floribert Chebeya Reuters

Faili la kesi ya mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC aliyeuawa mwaka 2010 kwenye mazingira ya kutatanisha limeibiwa kwenye ofisi ya waliki anayefuatilia kesi hiyo.  

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika lisilo la kiserikali la Voice of the Voiceless imesema kuwa usiku wa kuamkia siku ya alhamisi watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi walivamia ofisi ya mwanasheria Jean-Marie Kabangela Ilunga na kuiba nyaraka za kesi ya mwanaharakati Floribert Chebeya na dereva wake Bazana Faithful aliyepotea baada ya tukio.

Shirika hilo limesema kuwa toka juma moja lililopita, wakili Jean-Marie amekuwa akipokea simu kutoka kwa watu wasiojulikana ambao wamekuwa hawazungumzi pindi akipokea simu.

Shirika hilo limeonesha wasiwasi wake kuhusu usalama wa wanasheria ambao wanafuatilia kesi ya mauaji ya Chebeya na dereva wake ambapo aliuawa kwenye mazingira ya kutatanisha wakati akienda kuonana na Jenrali John Numbi ambaye ameachiwa.

Hivi karibuni mahakama ya kijeshi ilisikiliza upya kesi hiyo na kumkuta hana hatia Jenerali Numbi ambaye alikuwa mkuu wa polisi wakati huo na kudai kuwa hakuwahi kuwa na makubaliano ya kukutana na mwanaharakati Floribert Chebeya.

June 23 mwaka 2011 mahakama ya kijeshi nchini DRC ilimuhukumu adhabu ya kunyongwa Kanali Mukalay ambaye alikuwa ni kaimu mkuu wa polisi pamoja na maofisa wengine watatu kifungo cha maisha jela na kuwaachia wengine watatu.

June 19 2012 wakati kesi hiyo ikisikilizwa kwenye mahakama ya kijeshi iliingiliwa kati kabla ya May 7 kesi hiyo kuahirishwa kufuatia maagizo ya mahakama ya katiba nchini humo kutaka kesi hiyo kupitiwa upya kutokana na mapungufu.