RWANDA-UINGEREZA

Raia 4 wa Rwanda wakamatwa nchini Uingereza kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya kimbari, 1994

Raia watano wa Rwanda wamekamatwa na polisi wa Metropolitan nchini Uingereza kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini mwao mwaka 1994.

Moja ya makaburi ya Rwanda baada ya machafuko ya mwaka 1994
Moja ya makaburi ya Rwanda baada ya machafuko ya mwaka 1994 Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kukamatwa kwa watuhumiwa hao watano rais wa Rwanda kunakuja kufuatia ombi la mwendesha mashataka mkuu wa Serikali kuomba mahakama nchini Uingereza kuruhusu raia hao kurejeshwa nyumbani kukabiliana na kesi zao.

Mwaka 2009 raia hao walishinda kesi kwenye mahakama kuu nchini Uingereza ambapo jaji aliyekuwa akisikiliza shauri lao, alidai kuwa hawawezi kurejeshwa nchini mwao kutokana na hatari iliyopo kuhusu maisha yao.

Watuhumiwa hao waliiomba mahakama kutokubaliana na upande wa serikali kutaka warejeshwe nyumbani kwakuwa wanaamini hawatatendewa haki kutokana na jinsi kesi za watuhumiwa wengine zimekuwa zikiendeshwa ambapo kwa pamoja wamekana kuhusika na mauaji hayo.

Watuhumiwa wote isipokuwa Mutabaruka wamekamatwa kuhusiana na kesi yao ya awali ambayo walishinda na sasa Serikali ya Uingereza inajaribu kuwarejesha tena nchini mwao.

Raia hao wametajwa kuwa ni Emmanuel Ntezirayo, Charles Munyaneza, Celestine Ugirashebuja, Dr. Vincent Bajinya na celestine Mutabaruka.

Raia hao wanatuhumiwa kwa kuwa mstari wa mbele kwenye kuamrisha kutekelezwa kwa mauaji kati ya wahutu na watusi ambapo watu zaidi ya laki nane waliuawa ndani ya siku mia moja pekee.

Mwanasheria mkuu wa Serikali, Martin Ngoga amepongeza kukamatwa kwa watuhumiwa hao na kuongeza kuwa anaamini safari hii, mahakama ya Uingereza itakubaliana na ombi lake la kutaka watuhumiwa wote warejeshwe nchini mwao.