Brazili

Polisi wakabiliana na waandamanaji nchini Brazili

Polisi wa kutuliza ghasia wakiwa tayari kukabiliana na waandamanaji
Polisi wa kutuliza ghasia wakiwa tayari kukabiliana na waandamanaji AFP

Polisi nchini Brazili wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji nje ya uwanja wa Maricana wakati wa fainali za michuano ya soka ya kombe la mabara zilizotamatika mjini Rio De Janeiro. 

Matangazo ya kibiashara

Licha ya ghasia hizo mechi kati ya Brazili na Uhispania ilitamatika kwa wenyeji kupata ushindi wa mabao 3 kwa bila dhidi ya wapinzani wao ambao ni mabingwa wa dunia.

Mapema kabla ya kuanza kwa mechi hiyo waandamanaji walikabiliana na polisi katika majengo ya chama cha soka cha nchini humo CBF wakiilalamikia serikali kwa kutumia fedha nyingi katika maandalizi ya michuano hiyo na ile ya kombe la dunia ya mwaka ujao.

Maelfu ya wananchi wa Brazil wanaendelea na maandamano hayo kwa takribani mwezi mmoja sasa wakiishinikiza serikali kupunguza gharama za maisha