Australia

Waziri mkuu mpya wa Australia atangaza baraza lake la mawaziri

Waziri mkuu wa  Austrália Kevin Rudd
Waziri mkuu wa Austrália Kevin Rudd REUTERS/Andrew Taylor

Waziri Mkuu mpya wa Australia Kevin Rudd ametaja baraza lake la mawaziri hii leo likiwa na idadi kubwa ya wanawake kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo. 

Matangazo ya kibiashara

Akitangaza baraza hilo baraza hilo Rudd amesema uteuzi huo umezingatia uwazi na usawa wa jinsia na amewasiku kuchapa kazi kwa umakini katika kuhakikisha uchumu wa Taifa hilo unasonga mbele.

Wanawake walioingia katika baraza jipya ni wanane tofauti na tisa waliokuwa hapo awali katika serikali ya Waziri Mkuu aliyepita Julia Gillard.

Baraza hilo jipya linatarajiwa kuapishwa mapema leo jumatau na kuendesha kikao chake cha kwanza hii leo.