TANZANIA-MAREKANI

Obama ahitimisha ziara yake nchini Tanzania, azindua mradi mkubwa wa umeme

Rais Obama akiwa na mkewe Michelle wakijiandaa kuondoka Tanzania
Rais Obama akiwa na mkewe Michelle wakijiandaa kuondoka Tanzania

Rais wa Marekani Barck Obama amehitimisha ziara ya siku mbili nchini Tanzania, kama sehemu ya ziara yake ya siku saba Barani Afrika iliyoanzia nchini Senegal, Afrika Kusini na hatimaye Tanzania. 

Matangazo ya kibiashara

Katika ziara yake nchini Tanzania Barack Obama alipata nafasi ya kuzungumza na mwenyeji wake kwenye mazungumzo ya faragha ikulu jijini Dar es Salaam jana na kisha kuzungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari ambao walipata nafasi ya kumuuliza maswali kabla ya kushiriki dhifa ya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali ya Tanzania majira ya jioni.

Aidha mapema hii leo kabla ya kuelekea katika mtambo wa kuzalisha umeme ulioko Ubungo jijini Dar es Salaam, rais Obama na mtangulizi wake Gorge W Bush walifika kwenye ubalozi wa Marekani nchini Tanzania na kuweka mashada ya maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya watu waliouwawa katika shambulizi la kigaidi kwenye ubalozi wa Marekani nchini Tanzania mwaka 1998.

Ifuatayo ni Ripoti maalum iliyoandaliwa na Victor Robert Wile ambaye alikuwa akifuatilia ziara ya rais huyo wa Marekani.