AFRIKA KUSINI-MANDELA

Mahakama yamwamuru mjukuu wa Mandela kurejesha mabaki ya miili ya watoto wa Mandela

REUTERS/Rogan Ward

Mahakama nchini Afrika Kusini imemwamuru mjukuu wa mjukuu mkubwa wa Mzee Nelson Mandela Madiba, Bwana Mandla Mandela kurejesha mabaki ya miili ya watoto watatu wa rais wa zamani wa nchi hiyo Nelson Mandela.Mandla alikuwa anatuhumiwa na familia ya Mzee Mandela kuwa alifukua makaburi ya watu hao akiwemo baba yake na kwenda kuyazika katika eneo la karibu na makazi yake.

Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo lilifanyika miaka miwili iliyopita ambapo Mandla aliyahamisha mabaki hayo kutoka katika makaburi ya familia na mahakama imeamuru zoezi la kurejesha mabaki hayo lifanyike Jumatano.
 

Mpaka sasa haijulikani kama wanasheria wa Mandla Mandela watakata rufaa katika Mahakama Kuu katika Jimbo la Mashariki nchini humo.
 

Hatua hii inakuja wakati huu Mzee Nelson Mandela hali yake ikiwa mahututi huku wananchi wa Afrika Kusini wakiendelea kumwombea mzee Mandela.
 

Mandela yuko Hospitali akiwa mahututi akisumbuliwa na ugonjwa wa maambukizi katika mapafu uliosababisha hali yake kudhoofika.