SYRIA-URUSI-UN

Urusi yalitilia ngumu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Syria

REUTERS/Maxim Shemetov

Urusi imetilia ngumu matakwa ya Baraza la usalama la umoja wa mataifa kuwa Syria iruhusu mara moja kufikiwa kwa maelfu ya Raia waliokwama kutokana na Mashambulizi yanayofanywa na Serikali mjini Homs.Wanadiplomasia wanasema kuwa upinzani wa Urusi dhidi ya mapendekezo yaliyotolewa na Australia na Luxembourg ni ishara mpya ya kushika kasi ya mgawanyiko ndani ya Jumuia ya kimataifa juu ya Mzozo wa Syria.

Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataia, Ban Ki Moon juma hili alionesha hofu ya kuwapo kwa Raia takriban 2500 ambao wako katika hali ya sintofahamu mjini Homs , Huku Ofisi inayoshughulikia misaada ya kibinaadam imesema ina dawa kwa ajili ya Waathirika wa mapigano hayo isipokuwa wanashindwa kuwafikia.

Urusi, Mshirika mkuu wa Syria,pia iliwahi kukataa kuunga mkono wito uliotolea mwezi uliopita kuingia katika mji wa Qusayr uliokuwa ukidhibitiwa na Waasi mpaka pale Serikali iliporejesha mji huo katika himaya yake.

Australia na Luxembourg ilipendekeza hilo katika hatua ya kusisitiza wito wa Katibu Mkuu Ban Ki Moon aliyoitoa sambamba na Ofisi ya kuratibu Maswala ya Misaada ya Kibinaadam OCHA.

Urusi na China zimetumia nguvu zao kwa kura ya turufu wakiwa Wanachama wa kudumu wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya Maazimio matatu ambayo yameonekana yanamshinikiza Rais Bashar Al Assad.