MAREKANI-URUSI-ECUADOR

Matumaini ya Snowdern kupata hifadhi yaongezeka

Milango yafunguka kwa Edward Snowden,kupata hifadhi kwa mataifa kadhaa ya Amerika kusini.
Milango yafunguka kwa Edward Snowden,kupata hifadhi kwa mataifa kadhaa ya Amerika kusini. The Guardian

Hatimaye Matumaini yameongezeka kwa Edward Snowden huenda akaweza kuondoka moscow ambapo amekwama kwa siku 14 baada ya mataifa matatu ya Amerika kusini kujitolea kumuhifadhi baada ya kuvujisha siri za intelijensia ya Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Bolivia imekuwa nchi ya tatu kujitolea siku kumuhifadhi Edward Snowdern huku raisi wa nchi hiyo Evo Morales akisema yupo tayari kumuhifadhi snowdern kama akihitaji.

Nafasi hiyo inajitokeza ikiwa si muda mrefu tangu raisi wa venezuela Nicolas Maduro kujitolea hifadhi sambamba na raisi wa Nicaragua Daniel Ortega ambaye alisema nchi yake ingeweza kumpa hifadhi salama Edward snowden.

Mlolongo wa nafasi za kupata hifadhi unamiminika ikiwa ni baada ya mfululizo wa kukataliwa na mataifa mengi kati ya 21 ambayo Snowdern aliomba hifadhi juma lililopita.