Latvia

Latvia yakubaliwa kuwa mwanachama wa nchi zitumiazo Sarafu ya Euro

Waziri Mkuu wa Latvia,Valdis Dombrovskis
Waziri Mkuu wa Latvia,Valdis Dombrovskis

Nchi ya Latvia imekubaliwa na Umoja wa Ulaya na kuwa nchi mwanachama wa 18 wa jumuia ya nchi zinazotumia sarafu ya Euro kuanzia mwaka ujao.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imeelezwa na Waziri Mkuu wa LatviaValdis Dombrovskis kuwa ni siku njema kwa Latvia na pia kwa Ulaya, Baraza la ECOFIN linaloundwa na Mawaziri wa Uchumi na Mawaziri wa Fedha walitoa kibali hicho kwa Latvia
 

ilikuwa safari ndefu kwa Latvia tangu ilipojiunga na Umoja wa Ulaya mwaka 2004.
Dombrovskis amesema kuwa ingawa kumekuwepo na Changamoto ndani ya Umoja wa Ulaya, kuwa Mwanachama wa jumuia ya nchi zinazotumia Sarafu ya Euro, kutawaletea faida hasa katika suala la riba ndogo, na kuongezeka kwa uwekezaji wa nchi za kigeni.
 

Latvia imesema kuwa inaamini Umoja wa Ulaya na Jumuia inayotumia sarafu ya Euro na kuwa itathibitisha mataifa mengine kuwa mmoja kati ya Wanachama wanaofanya vizuri ndani ya Umoja huo.
 

Latvia iliibuka mwaka 2008-09 kuwa nchi ambayo uchumi wake unakua kwa kasi na pato lake la taifa lilikua kwa zaidi ya ya ailimia tano mwaka hadi mwaka kwa kipindi cha mwaka 2011 na 2012.

hata hivyo Waziri mkuu wa Latvia anasema wanakabiliwa na Changamoto ya kukubalika kwa nchi hiyo kuingia ndani ya jumuia ya nchi zinazotumia Sarafu ya Euro.
 

Kwa Mujibu wa matokeo ya kura za maoni zilizopigwa zinaonesha kuwa asilimia 53 ya Raia wa Latvia wamekataa kujiunga kwenye jumuia hiyo huku asilimia 22 ikiridhia, huku asilimia nyingine 25 hawakuamua chochote.