Ireland

Wabunge nchini Ireland waunga mkono muswada wa Sheria kuruhusu utoaji mimba nchini humo

Rais wa Ireland, Michael Higgins
Rais wa Ireland, Michael Higgins

Wabunge nchini Ireland mapema Ijumaa hii wamepitisha mswada wa kuridhia utoaji mimba kwa wanawake kitu ambacho kitafanyika kwa kuangalia sababu kadhaa zikiwemo hatari anayokabiliana nayo mama mjamzito.

Matangazo ya kibiashara

Mswada huo umepigiwa kura ya ndiyo na wabunge mia moja ishirini na saba huku wabunge thelathini na moja pekee wakipinga kupitishwa kwake wakidai taifa hilo linaweza likawa limeingia kwenye mpango wa kubariki utoaji wa mimba kwa wanawake.

Mswada huo sasa unapelekwa kwenye Baraza la Seneti na kama utapitishwa basi itakuwa jukumu la Rais kusaini ili uwe sheria na umekuja baada ya mwanamke raia wa India Savita Halappanavar kufikwa na umauti kutokana na matatizo ya ujauzito aliokuwa nao.

Muswada huo ulipitishwa kaw kura 127 dhidi ya 31 baada ya siku mbili za mjadala mkali ndani ya Bunge.

Katika mchakato huo, Waziri mdogo amejiuzulu wadhifa wake baada ya kupiga kura ya kutounga mkono muswada huo ambapo anatarajiwa kuondolewa katika Baraza la Mawaziri wa Chama kinachotawala Fine Gael, Chini ya Waziri Mkuu Enda Kenny.
 

Waziri mdogo anayeshughulikia maswala ya Ulaya, Lucinda Creighton amesema kua anasikitika kupiga kura ya kutounga mkono Muswada wa Sheria kuruhusu utoaji mimba.
 

Kenny ameweka wazi kuwa hivi karibuni alipokea Barua za kumkashifu zikiwa zimeandikwa kwa Maandishi ya Damu huku waliokuwa wakipinga muswada huo wamemuita Waziri huyo muuaji.
 

Muswada unaosisitiza uhai awkati wa kipindi cha uja uzito, unaruhusu Mimba kutolewa katika Mazingira ambayo Matabibu watathibitisha na kuidhinisha kuwa kuna hatari ya maisha ya mama wakati wa ujauzito.