MISRI

Marekani yalitaka jeshi la Misri kumwachia huru Mohamed Morsi

Rais aliyeondolewa madarakani nchini Misri Mohamed Morsi
Rais aliyeondolewa madarakani nchini Misri Mohamed Morsi www.csmonitor.com

Marekani imetoa wito kwa jeshi la Misri kumwachia huru rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi, huku makumi kwa maelfu ya wafuasi wake wakiapa kuendelea kupigana kwa ajili ya kurejeshwa kwake madarakani. 

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Ikulu Jen Psaki amesema kuwa Marekani imekubaliana na wito wa awali wa Ujerumani kuhusu kuachiwa huru kwa Morsi na sasa inatoa wito huo huo hadharani.

Morsi ambaye aliondolewa madarakani mnamo July 3 amehifadhiwa mahali salama kwa mujibu wa viongozi wa mpito wa serikali ya Misri na hajaonekana hadharani tangu kupinduliwa kwake.

Psaki amesema kuwa Washington inataka kukomeshwa kwa vikwazo dhidi ya wapi alipo Mohamed Morsi wakati Ujerumani imependekeza taasisi inayoaminiwa kama vile Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu ICRC iruhusiwe kumfikia.