SYRIA

Umoja wa Mataifa wahofia usalama wa raia kwenye mji wa Homs nchini Syria

Shambulizi la guruneti mjini Homs
Shambulizi la guruneti mjini Homs REUTERS/Maysara Al-Masri/Shaam News Network/Handout via Reuters

Umoja wa mataifa umesema kuwa silaha za aina mbalimbali na vifaru vimeendelea kutumika katika mashambulizi yanayozidi kuwa mabaya siku hadi siku katika mji wa Homs nchini Syria jambo linalotishia usalama wa raia. 

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa shughuli za msaada wa kibinadamu wa umoja huo Valerie Amos na mkuu wa haki za binadanu Navi Pillay wametoa wito mpya wa kufikiwa kwa mji wa Homs lakini vikosi vya Rais Bashar al-Assad na waasi wa upinzaniwamekuwa wakikataa kuwapa uhakika juu ya usalama wao.

Umoja wa Mataifa na Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) wamesema wako tayari kukimbiza misaada ya kibinadamu kama ingewezekana kuzuia mapigano.