SYRIA

Jeshi huru la Syria laomba msaada wa silaha toka jumuiya ya kimataifa

REUTERS/Khalil Ashawi

Jeshi huru la Syria FSA limeomba msaada wa silaha toka jumuiya ya kimataifa ili liweze kukabiliana vyema na wapiganaji wenye uhusiano na kundi la kigaidi duniani la al-Qaeda, ombi hilo limekuja siku moja baada ya kuuawa kwa viongozi wa juu wa FSA.

Matangazo ya kibiashara

Mauaji hayo yametajwa kuongeza hofu katika jeshi hilo ambalo inasemekana huenda likaambulia patupu kama halitapatiwa msaada zaidi kwani Rais Assad emeendelea kuungwa mkono na baadhi ya makundi ya wapiganaji wa nje ya Syria wanaokinzana na sera za kimagharibi.

Wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu waliopo nchini humo wameafiru kuwa kundi la Hezbollah la nchini Lebanoni limeendelea kupambana na waasi wanaopingana na Rais Assad.

Wakati hayo yakijiri, mashambulizi makali yameendelea kushuhudiwa katika mji wa Homs kati ya vikosi vya serikali Rais Bashar a-Assad na wapinzani kwa zaidi ya majuma mawili sasa.

Shirika la msalaba mwekundi limetoa wito kwa pande zote kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia wahanga wa mapigano katika eneo hilo.