SUDANI-TANZANIA

Miili ya wanajeshi saba wa Tanzania inatarajiwa kuwasili leo jijini Dar es Salaam

Miili ya wanajeshi raia wa Tanzania inatarajiwa kuwasili jumamosi jijini Dar Es Salaam tayari kwa mazishi
Miili ya wanajeshi raia wa Tanzania inatarajiwa kuwasili jumamosi jijini Dar Es Salaam tayari kwa mazishi www.facebook.com

Miili ya wanajeshi saba wa jeshi la Umoja wa Afrika raia wa Tanzania ambao waliuawa kufuatia shambulio huko Darfur inatarajiwa kuwasili leo jijini Dar es salaam tayari kwa taratibu za mazishi.

Matangazo ya kibiashara

Wakati taratibu za maziko zikiandaliwa mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC Fatou Bensuda ametoa onyo kali kuhusu shambulizi la hivi karibuni lililowalenga waangalizi wa amani kutoka umoja wa mataifa na jeshi la umoja wa afrika huko Darfur sudan na kusema kuwa linaweza kuhesabika kama uhalifu wa kivita.

Katika taarifa yake akiwa Heague Fatou Bensuda amekumbusha pande zote zenye mgogoro kufahamu kuwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ina mamlaka jimboni Darfur.

Hivi karibuni wanajeshi walinda amani saba raia wa Tanzania waliuawa na wengine kumi na saba kujeruhiwa baada ya shambulizi kutekelezwa na kundi ambalo halijafahamika huko Darfur mnamo tarehe 13 mwezi Julai.