ZIMBABWE

Waziri Mkuu wa Zimbabwe Tsvangirai atoa onyo kwa Tume Huru ya Uchaguzi kuhakikisha Uchaguzi unakuwa Huru na Haki

Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai akiwa kwenye kampeni za kinyang'anyiro cha ucahguzi wa rais
Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai akiwa kwenye kampeni za kinyang'anyiro cha ucahguzi wa rais REUTERS/Philimon Bulawayo

Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai ametoa onyo kwa Tume Huru ya Uchaguzi nchini humo ZEC kuhakikisha uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu unakuwa huru na haki kinyume na hapo Taifa hilo huenda likaingia kwenye machafuko.

Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Tsvangirai ameitoa kwenye kampeni zake za uchaguzi alizofanya katika Jiji kla Harare na kuweka bayana Tume Huru ya Uchaguzi ZEC ndiyo ambayo itaingia lamani iwapo kutakuwa na wizi wa kura ambao umeshuhudiwa kwenye chaguzi zilizopita.

Tsvangirai amewaonyoshea kidole cha lawama maofisa wa Tume Huru ya Uchaguzi ZEC kwamba wao ndiyo wenye uwezo wa kuliepusha taifa hilo na machafuko iwapo watasimama kidete kuhakikisha uchaguzi huo unakuwa huru na haki.

Maelfu ya wafuasi wa Tsvangirai walihudhuria mkutano huo wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Gweru ambao Kiongozi wao huo wa Chama Cha MDC alitumia muda wake mingi kuonesha wasiwasi wa uwepo wa njama za wizi wa kura.

Kiongozi huyo wa Chama Kikuu Cha Upinzani nchini Zimbabwe cha MDC amesema wakati umefika kwa maofisa wa ZEC kuwa wakeli na kuhakikisha uachaguzi huo unakuja na matokeo kulingana na wananchi walivyoamua.

Tsvangirai ameweka bayana wafuasi wake hawatakuwa na uvumilivu pale ambapo wataona kabisa kuna wizi wa kura ambao unalenga kumsaidia Rais Robert Gabriel Mugabe aweze kushindwa kwenye kinyang'anyiro hicho cha tarehe 31 mwezi Julai.

Kwa upande wake Rais Mugabe akiendelea na kampeni zake amewataka wafuasi wake kuendelea kukiamini chama tawala cha ZANU-PF ili kiweze kuendelea kupambana na maadui wa kisiasa waliopo katika ardhi hiyo.

Rais Mugabe amesema hawawezi kuiweka nchi hiyo rehani kwa kuwakabidhi Viongozio ambao ni vibaraka wa mataifa ya magharibi wanaotaka kuona wananchi wa taifa hilo wakiendelea kuteseka na wao wanufaike na rasilimali.

Kinara huyo wa ZANU-PF Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 89 amesema mapambano yataendelea na huu ni wakati wa kuhakikisha wananchi wanaendelea kunufaika na rasilimali zao zilizowafanya wapiganie uhuru wao.

Uchaguzi Mkuu nchini Zimbabwe umepangwa kufanyika tarehe 31 mwezi Julai lakini tayari Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC imetoa wito wa kufanyika kwa uchaguzi huru na haki.