AFRIKA KUSINI

Afya ya Nelson Mandela yatajwa kuzidi kuimarika licha ya kuendelea kusalia mahtuti akipatiwa matibabu huko Pretoria

Bango lenye picha ya Rais wa Kwanza Mzalendo nchini Afrika Nelson Mandela likiwa nje ya Hospital anayopatiwa matibabu
Bango lenye picha ya Rais wa Kwanza Mzalendo nchini Afrika Nelson Mandela likiwa nje ya Hospital anayopatiwa matibabu Reuters / Mukoya

Afya ya Rais wa Kwanza Mzalendo na Mpambanaji wa dhidi ya Ubaguzi wa Rangi nchini Afrika Kusini Nelson Mandela maarufu kama Mzee Madiba imeendelea kuimarika kipindi hiki akiendelea kupatiwa matibabu ya mapafu kwa majuma zaidi ya sita.

Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma imeweka bayana japokuwa Madiba bado yupo mahututi lakini afya yake imeendelea kuimarika kila siku tofauti na ilivyokuwa hapo awali kitu ambacho kinaongeza matumaini ya kutoka Hospital akiwa mzima.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Ofisi ya Rais Zuma imewaondoa hofu maelfu ya wananchi wa Afrika Kusini ambao wamekuwa wakitaka kujua hali ya afya ya Kiongozi wao wa zamani na mpigani uhuru wa Taifa hilo.

Ofisi ya Rais Zuma pia imetoa shukrani za dhati kwa wananchi wote ambao walihusika kwa namna moja ama nyingine kwenye sherehe za kukumbuka siku ya kuzaliwa kwa Madiba wakati akitimza miaka 95 juma lililopita.

Taarifa hiyo imesema hatua ya wananchi wa Afrika Kusini kujitokeza na kufanyakazi kazi za kijamii kwa dakika sitini na saba kilionesha namna ambavyo wananchi wa Taifa hilo walivyotayari kumuenzi Baba wa Taifa Madiba.

Katika hatua nyingine Chifu wa Ukoo wa Mandila ambaye ni Mjukuu wake Mandla Mandela naye ametoa taarifa za kuimarika kwa afya ya Madiba anayeendelea kupatiwa matibabu ya maradhi ya mapafu huko Pretoria.

Mandla alitoa taarifa hiyo baada ya kutembelea Hospital aliyolazwa Madiba na kuweza kumuona kitu ambacho amesema kimeongeza matumaini kwa upande wake kuona wakati siyo mrefu atashuhudia Babu yake akitoa eneo hilo.

Madiba amekuwa akipatia matabibu kwa kipindi cha majuma zaidi ya sita kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya mapafu yanayotaja yalianza kumsumbua tangu alipokuwa anatumikia kifungo katika Kisiwa cha Robben.