ZIMBABWE

Muda wa kujisalimisha Waasi DRC wayoyoma

Makundi ya waasi yanayomiliki silaha mashariki mwa jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo yatakiwa kujisalimisha mara moja hadi ifikapo saa kumi alhamisi.
Makundi ya waasi yanayomiliki silaha mashariki mwa jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo yatakiwa kujisalimisha mara moja hadi ifikapo saa kumi alhamisi. RFI

Makundi yote ya Waasi yaliyoko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ,Jimboni Kivu ya Kaskazini yanasubiriwa Kujisalimisha na kutoa Silaha zao Hadi saa Kumi Hii leo Alhamisi. 

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Kikosi Hicho cha Umoja wa Mataifa,Charles Bambara anasema kwamba Muda wa saa Arobaini na Nane Uliotolewa Kwa Makundi ya Waasi kujisalimisha ,umeanza kupata Matunda na Kuitikiwa na Makundi ya Waasi.

Hata Hivyo kundi la Waasi la M23 lenyewe limetupilia mbali Wito huo na Kusema Kuwa wao Hawahusiki.

Mwenyekiti wa Kundi Hilo Bertrand Bisimwa amesema wao wanaendelea Kuiomba serikali kurudia mazungumzo ya Kampala na kuongeza kuwa Huu sio wakati wa vitisho.

Umoja wa Mataifa Huko Congo,Monusco Uliyatolea Muda wa Saa Arobaini na Nane kwa makundi hayo Kujisalimisha.

Jumatano Maofisa wakuu wa Monusco walitoa Ramani ya Maeneo ambayo Wanajeshi Elfu Tatu wa Kikosi Kipya cha Umoja wa Mataifa kitaanza kufuatilia Makundi ya waasi yenye silaha.