Uhispania

Waziri mkuu Uhispania kikaangoni,kufuatia kashfa ya ufisadi

Waziri mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy.
Waziri mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy. REUTERS/Sergio Perez

Waziri mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy amewakabili wabunge katika maswali na majibu yaliyolenga kashfa ya ufisadi inayotishia chama chake mashuhuri kilichopo madarakani PP.

Matangazo ya kibiashara

Waziri Rajoy atakabiliwa na maswali kuhusu malipo haramu yaliyofanywa na mhazina wa zamani wa chama chake Luis Barcenas ambapo awali waziri huyo na wanachama wengine walikanusha madai ya kupokea malipo haramu.

Hasira kali ilienea kufuatia madai hayo kugusa maeneo nyeti nchini Uhispania na kusababisha maandamano ya kupinga serikali na wito kwa waziri huyo kujiuzulu.

Hivi karibuni kulizuka mapigano kati ya polisi na waandamanaji waliokuwa wakipinga serikali mnamo katikati ya mwezi julai ambapo zaidi ya watu elfu moja walikusanyika nje ya ofisi za makao makuu ya chama cha PP na kukitaka kujiondoa madarakani.

Waziri Rajoy anajitokeza mbele ya bunge kufuatia vitisho vya kura ya kutokuwa na imani nae,katika maelezo yake ya awali alibainisha kuwa anajitokeza wakati huu kwa vile madai hayo hayana ukweli.