SYRIA

Upinzani nchini Syria waahidi kutoa ushirikiano kwa wakaguzi wa Umoja wa Mataifa UN wanaochunguza kutumika kwa silaha za kemikali

Viongozi wa muungano wa taifa wa Syria
Viongozi wa muungano wa taifa wa Syria in.reuters.com

Viongozi wa upinzani nchini Syria wamesema kuwa wapotayari kuwapa ushirikiano wakaguzi wa Umoja wa Mataifa UN ili kufika katika maeneo ambayo yako chini ya udhibiti wa waasi kuchunguza kutumika kwa silaha za kemikali. 

Matangazo ya kibiashara

Muungano wa Taifa wa Syria umesema katika taarifa yake kuwa inataka wakaguzi kwenda kwanza katika mji wa Khan al-Assal, ambapo mashambulizi yaliyofanywa kwa silaha za kemikali yaliripotiwa mnamo Machi 19.

Tangazo hilo limekuja baada ya timu ya Umoja wa Mataifa, wakiongozwa na mtaalam wa uswis Ake Sellstrom, kufikia makubaliano na serikali ya Rais wa Syria Bashar al-Assad kuingia nchini humo.